Simon Mbwana Mwakatobe maarufu mc Simon Mzungu ni kijana mwigizaji,mwimbaji kwaya ya vijana kanisa la K.K.K.T Kinyerezi na mshereheshaji (mc) katika matukio mbalimbali kama Harusi,send off na sherehe mbalimbali.Mc Simon Mzungu ni mwenyeji wa Mbeya amesoma shule ya msingi mbata na sekondari shule ya Sangu kabla ya kwenda Dar es salaam kusoma ufundi wa magari chuo cha NIT.Alianza kuvutiwa na kazi ya kuwa mshereheshaji (mc) Alipohudhuria harusi ya mjomba wake na marehemu David alivutiwa na mc wa siku hiyo na kujipa moyo siku moja atakuwa kama yeye.'Siku ya kwanza kusimama rasmi kama mc Nilialikwa sherehe ya Dada yangu mmoja,Nilipotokea wakaniambia Tumekosa mc simama Wewe basi tangu siku hiyo Nikaanza rasmi kama career yangu maana Walinisifu sana kwamba Wewe ni mc kabisaa'.Mpango Wangu sasa ni kutangaza brand yangu inayoitwa 'huduma bora ya nyota tano daima' ambayo ni huduma ya viwango bora kabisa Tanzania.Namshukuru Mungu mpaka sasa Namiliki kampuni yangu inayoitwa Amazing Simon Entertainment ambayo inajishughulisha na filamu,kuandaa sherehe na matamasha mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni