Jumatano, 8 Oktoba 2014

BARAKA NA EDNA!SHANGWE SHANGWE

Ilikuwa ni furaha,nderemo na vifijo wakati wa Harusi ya Baraka na Edna ambayo ilifanyika kanisa la Moravian segerea,na kufuatiwa na tafrija ambayo ilifanyika ukumbi wa Airwing bwalo C,mc Simon Mzungu Nilipata fursa ya kusherehesha harusi hii ambayo ilikutanisha makabila ya Kinyakyusa anapotoka Bwana harusi na Muha anapotoka Bibi harusi mambo yalikuwa bam bam Watu walicheza ikhangalamukaga na leka Dutigite.Bwana Harusi ni classmate Wangu Tulisoma pamoja shule ya msingi Mbata iliyopo Mbeya mjini na Tulimaliza pamoja.Ucheshi haukukosekana kwa kuwachekesha maharusi na Wageni waalikwa kwa ucheshi mzuri bila kumuuzi Mtu au kumkera.Wageni waalikwa walipata nafasi ya kupiga picha na maharusi,pamoja na kupata burudani nzuri ya muziki kutoka kwa Dj Ras wa Amazing Simon Entertainment (ASEN).Tunawatakia kheri na fanaka Bwana harusi Baraka na Malkia Edna katika maisha yao ya ndoa pamoja sana.
mc Simon Mzungu,Nikiwahoji maharusi kwa maswali mazuri ya ucheshi na kufurahisha wageni waalikwa kwa furaha na bashasha ilikuwa poa sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni