Ijumaa, 14 Machi 2014

MFALME DAUDI NA MALKIA ROSE!WASHEREHEKEA

Mfalme Daudi na Malkia Rose,walifunga pingu za maisha kanisa la K.K.K.T Kinyerezi na kufuatiwa na sherehe ambayo ilifanyika ukumbi wa Babylon resort uliopo kinyerezi mwisho,ilikuwa ni sherehe ambayo ilifana sana ukizingatia maharusi wote ni waimbaji wa kwaya ya K.K.K.T Kinyerezi kwaya ya Uinjilisti sherehe ilitawaliwa na uchangamfu wa hali ya juu.MC Simon Mzungu,Nilipata fursa ya kusherehesha sherehe hii kama kawaida 'Huduma bora ya nyota tano daima *****'  ambayo ni kauli mbiu ya Amazing Simon Entertainment (ASEN) Ilitoa burudani nzuri kwa wahudhuriaji wa sherehe hii.Bwana Harusi Daudi alipendeza kwa suti nyeusi na msaidizi wake,pamoja na malkia Rose aliyevaa shela yake nzuri.Rangi ya ukumbi ilikuwa ni blue na silver.Bwana harusi asili yake ni Dodoma wakati Bi harusi asili yake ni marangu kabila ni mchaga.Tunawatakia maisha mema ya ndoa yenu Mungu awabariki kwa kutupa nafasi ya kusherehesha harusi yenu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni